Watu wenye ulemavu wa kusikia hasa kina mama wajawazito mara nyingi hukosa kutembelea hospitali kupata huduma za utunzaji wa mimba kama watu wengine. Hii ni kutokana na hofu kwamba huwa vugumu kwao kuwasiliana na wahudumu wa afya na kuwaelewa mahitaji yao.
Ili kukabiliana na vikwazo vinavyowakabili kina mama wajawazito wanapotembelea hospitali kwa huduma hizo, serikali ya kaunti ya Kilifi ilianza kufadhili mafunzo ya wakalimani wa lugha ya ishara mwaka wa 2016.
Lengo likiwa ni kuwasaidia wanawake wenye ulemavu wa kusikia kuwasiliana na wahudumu wa afya wanapotafuta huduma za afya ya uzazi, na kuwawezesha kuuliza maswali na kuelewa kikamilifu taarifa zinazotolewa kwao.
Kama anavyosimulia Ruth Keah kwenye makala haya -Kutatua changamoto ya mawasiliano kwa wajawazito wenye ulemavu wa Kusikia.
By Ruth Keah