September 25th, 2023

Changamoto za kutunza Mimba Kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya

Challenges of maintaining pregnancy for drug addicts.
Changamoto za kutunza mimba kwa waraibu wa dawa za kulevya

| Athuman Luchi

Waraibu wengi wa madawa, wanapokuwa wajawazito, hushindwa kutembelea vituo vya huduma za afya, jambo linalosababisha vifo vya watoto wao na hata maisha yao wenyewe wakati wa kujifungua.

Salma Ismail, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa mtumiaji wa cocaine na Heroine kwa miaka mitatu, tangu mwaka 2019.

Watoto watatu wa Salma walifariki wakati alipokuwa mraibu wa mihadharati. Anasema kwamba wakati wa ujauzito wake, kamwe hakufikiria kutembelea vituo vya afya kwa huduma za uzazi kwa sababu akili yake ilikuwa imezama katika fikira za jinsi ya kupata madawa ya kulevya.

By Athuman Luchi